Fursa Tano Zinazopatikana Kwenye Ajira ukiacha Mshahara.
Labels:
EMPLOYMENT
,
SUCCESS
Katika kuzungumza na watu wengi kuhusiana na ajira na mshahara inaonekana watu wengi sana wanachoangalia kwenye ajira ni mshahara tu. Kuweka fedha kama lengo kuu la kufanya kazi ndio kunakosababisha kazi na maisha kuwa vigumu sana(soma; kama unafanya ili upate fedha maisha yako yatakuwa magumu sana)
Kuna fursa nyingi sana zinazopatikana kwenye ajira ukiacha mshahara. Kwa kuweza kuzigundua na kutumia fursa hizo utaboresha maisha yako na ya wanaokuzunguka.
Hebu tuone fursa tano zinazopatikana kwenye ajira tofauti na mshahara.
1. Uzoefu wa kazi. Hakuna kitu muhimu kwenye utaalamu wako kama uzoefu. Na siku zote uzoefu haupatikani darasani bali kwa kufanya vitu halisi. Hata usome vitu vingi kiasi gani unapofika wakati wa kutenda kuna changamoto nyingi. Hivyo kwenye ajira ni sehemu nzuri ya kupata uzoefu wa kazi hasa pale unapotoka masomoni. Uzoefu huu utakusaidia baadae kuweza kupata kipato kikubwa kwa kuajiriwa ama kujiajiri.
2. Kukuza mtandao wako. Kuna usemi “haijalishi unajua nini bali unamjua nani”. Haitoshi tu kujua vitu vingi bali unatakiwa kuwajua watu wengi wanaohusiana na unachofanya. Njia pekee ya kujuana na watu wengi wenye utaalamu kama wako ni kupitia ajira. Katika ajira unaweza kujuana na waajiri wengine na pia wadau mbalimbali wanaohusiana na kazi unayoifanya. Kwa mtu anayejua kuutumia mtandao, ndani ya mwaka mmoja wa kazi atakuwa amepata fursa nyingi kuliko aliyejifungia nyumbani akisubiri kazi ya mshahara mkubwa.(soma; haijalishi unajua nini bali unamjua nani.)
3. Kuweza kuishi na kufanya kazi na watu wa aina mbalimbali. Unaweza kuchukulia rahisi sana ila hakuna kitu kigumu kwenye ajira kama kuweza kufanya kazi na watu wenye tabia tofauti tofauti. Chanzo kikuu cha msongo wa mawazo kazini unatokana na kushindwa kuchangamana au kuelewana na wafanyakazi wengine. Tafiti zinaonesha sababu kuu ya watu kuacha, kufukuzwa ama kazi kuwa ngumu kunatokana na kutoweza kuendana ama kuelewana na wafanyakazi wengine. Kwenye ajira kuna changamoto nyingi sana zinazotokana na tabia za watu. Kuna wenye majungu, kuna wa kujipendekeza kwa bosi, kuna wanaopenda kuonekana wao ndio wanajua sana na mengine mengi. Kuweza kufanya kazi vizuri na watu kama hawa bila ya wewe kupata msongo wa mawazo ni uzoefu tosha wa wewe kuweza kuwa kiongozi mzuri.
4.Kuonesha uwezo wako na vipaji vyako. Kila mtu ana uwezo mkubwa sana uliopo ndani yake. Kila mtu anavipaji vya kipekee vinavyomtofautisha na watu wengine. Kila mtu ana ubunifu mkubwa. Kwa kupata kazi na kisha ukaonesha vitu hivi vya kipekee ulivyonavyo ni rahisi sana kupata kipato kikubwa na nafasi nzuri. Kwa sababu kwa kutumia upekee wako utafanya kazi vizuri na kwa utofauti mkubwa. Hii itafanya kila mtu afurahie kazi yako na hii itakuletea furaha kubwa.(soma; hiki ndio chanzo kikuu cha wewe kukosa furaha)
5. Kuanza kufanya mazoezi ya mafanikio kwa kuhudhuria/kuonekana kila siku. Kumbuka mafanikio ni kuhudhuria/kuonekana kila siku. Yaani lazima uwe na tabia ya kufanya vitu vinavyokuletea maendeleo kila siku bila kuchoka. Tabia hii ya kufanya vitu kila siku bila kuchoma ama kukata tamaa unaweza kujifunza kwa kuangalia maisha ya kwenye ajira yalivyo. Hata kama umeamka asubuhi, umechoka choka na hujisikii kufanya kazi siku hiyo bado itakulazimu kwenda kazini. Kwa kuweza kuhamishia tabia hiyo kwenye mambo yako binafsi itakuwa rahisi sana kwako kufanikiwa.(soma; hii ndio gharama ya mafanikio unayotakiwa kulipa)
Kama upo kwenye ajira ama ndio unajiandaa kuingia kwenye ajira badili mtizamo wako juu ya ajira na mshahara. Usiangalie sana mshahara bali angalia fursa nyingine na jinsi unavyoweza kuzitumia kufikia malengo yako.
Kama unalengo la kujiajiri hutoweza kufanya hivyo kwa kuangalia mshahara, na hiyo ndio sababu inayowafanya wengi washindwe kujiajiri. Uzoefu wa kazi, mtandao na kuweza kufanya kazi na watu wa aina mbalimbali ni vitu muhimu sana pale unapojiajiri.

0 maoni:
Chapisha Maoni