| MWINJILISTI MWAKILIMA ATAHUBIRI |
Injili ya Yohana ina idadi kubwa tu ya ahadi za Yesu kuhusu nafasi ya Roho Mtakatifu katika maisha ya waaminio. Hebu tusome baadhi yake.
Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele. Ndiye Roho wa kweli, ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui. Bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. - (Yohana 14:16, 17).
Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia (Yohana 14:26).
Lakini mimi nawaambia iliyo kweli – yawafaa ninyi mimi niondoke. Kwa maana, mimi nisipo-ondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu, bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. … Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa. Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote. Kwa maana, hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.
Na yote aliyo nayo Baba ni yangu, kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasheni habari (Yohana 16:7; 12 – 15)