Alhamisi, 7 Novemba 2013

NINI MAANA YA WOKOVU

Unknown | 07:54 |

ASKOFU  SPEAR MWAIPOPO

“Kwasababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako yakuwa Mungu alimfufua katika wafu, UTAOKOKA. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa mtu hukiri hataKUPATA WOKOVU”. (Rum 10:9-10.)


Baada ya kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako, ni muhimu sana kupata mafundisho ya awali, yatakayokusaidia kujua kwa hakika, maana ya KUOKOKA au WOKOVU;


“ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.” (Efe 4:14)

Ndio maana Yesu alisema, tukishawahubiri na kuwasaidia kuokoka,tuwafundishe yote!“Yesu akaja kwao akasema nao, akawaambia, nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na mkiwafundisha kuyashika yale yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote hadi ukamilifu wa dahari”. (Math 28:18-20).
“Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye; wenye shina na wenye kujengwa katika yeye;mmefanywa imara katika imani, kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani”. (Kol 2:6-7)


“Wakawa wakidumu katika fundisho la Mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali” (Mdo 2:42)
“Muwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu, lakini kwa upole na kwa hofu” (1Pet 3:15)
Share this article

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Copyright © 2015 HEZRON MWANAFUNZI WA YESU • All Rights Reserved.
Blogger Templates Design by BTDesigner • Powered by Blogger