Kujiunga
Beep Mara moja tu Kwenye no 0755 700 820 utapokea ujumbe wa maelekezo
Kuwaimarisha vijana kwenye Neno kwa njia
mbalimbali za kuwafundisha, kufanya MAKONGAMANO Semina na mashindo
yanayoweza kuibua vipawa na karama pamoja na maarifa Mungu Aliyoweka
ndani yao, kutoa zawadi za pesa taslimu au vifaa ili kutia moyo vijana
waamshe shauku yao ya kusoma Neno na kulitafakari.
Kufikia nchi nzima ya Tanzania kupitia vijana waliookoka ili nao wawalete wengine kwa Yesu.
Kuanzisha mahubiri kwenye kila
daladala/mabasi yote yanayofanya safari ndani ya nchi hii,kwa kuwa
matatizo mengi yaliyomzunguka mwanadamu yanasababishwa na dhambi Rumi
2:9-11, hivyo kwa kutumia rasilimali watu vijana wenye ufahamu mzuri
hawa watakuwa waalimu, wainjilisti (wahubiri) wasimamizi wa miradi
itakayo anzishwa ili kupiga vita Dhambi ufukara na Ujinga.
Kuhubiri Injili Kwa Njia ya Techkohama (ICT)
kuazisha tovuti na database kwa kila
Kanisa na kumwaandaa kijana mmoja atakayeisimamia, na kuingiza
kumbukumbu pamoja na kutoa ripoti wakati zinapohitaji. Mchungaji wa
Kanisa la mahali pamoja ndiye atakayekuwa msimamizi mkuu kwa kuhakikisha
kila kitu kipo sawa kabla ya kuwekwa hewani hasa data zote za website.
Kuitumia website (Mtandao) kuwa chombo cha kupeleka Injili kwa kasi na
kufikia vijana wa kizazi kipya cha dot com, Injili ni uweza wa Mungu
hivyo unaweza kumfikia kila mtu na mahali popote na kwa wakati wowote,
mimi na wewe tunawajibika kuipeleka Injili kwa kila mtu, tunahitaji
taaluma na Bwana kaiweka mikononi mwetu, tuitumie ili kutimiza malengo
ya Mpango Mkakati wa Miaka Kumi Ya Mavuno Tanzania. Kutakuwa na website
za aina mbili, (1.) Isiyo na gharama ila backup ya kila mwezi (2.) Yenye
gharama kulingana na hitaji la Kanisa husika.
Huduma
Kwanza ningependa kusema kuwa
hatuanzishi jambo jipya, bali ni kuboresha na kuongeza kasi kwenye
huduma ya kuwafikia watu kwa Injili ya Yesu, kwa ubora, ubunifu na
utaalamu wa hali ya juu.
kutembelea wagonjwa, wafungwa na wajane
na Yatima. Kufikia mashule na vyuo kwa Injili ya Yesu na mengine mengi
kwa kadri ya Neema ya Bwana, Huduma hii itafanya kwa kushirikiana na
Kanisa la mahali kupitia idara ya vijana woca watakuwa wawezeshaji
kuhakikisha lengo linatimia.
Uaminifu – kuifanya huduma hii
kunahitaji uaminifu kwa Mungu na kwa wanadamu kwa kutumika bila kujali
hali,mazingira wala muda, bali kujitoa kwa moyo na kwa nia iliyosafi,
kitu ambacho kimekuwa mtihani mgumu kwa wengi.
Kutoa Ujunzi
Kufungua vyuo vya mafunzo ya ufundi kila
jimbo, Section na Kwenye Kanisa la mahali kulingana na uhitaji wao, ili
kutoa fursa kwa Vijana kujifunza na kukabiliana na soko la ajira
duniani.
Maombi saa:
6:00 hadi 7:00 mchana
9:00 hadi 10:00 jioni
12:00 hadi 1:00 usiku
9:00 hadi 11 alfajiri Kila siku
Mkesha saa 5:00 usiku hadi 9:00 Alfajiri kila ijumaa
0 maoni:
Chapisha Maoni