Ijumaa, 25 Oktoba 2013

Unknown | 23:41 |

KWA WALE WANAOPENDA KUWASEMA VIBAYA WATUMISHI WA MUNGU

Ukimsema vibaya mtumishi yeyote wa Mungu, ikatokea yule mtumishi amepakwa mafuta na Mungu kweli utashiriki laana ya kumsema vibaya, na hutaweza kupokea hata nusu ya uweza wa mtu yule.

Kumsema mwingine vibaya ni uthibitisho kuwa mtu huyo amekuzidi, na ndio maana Mfalme Daudi alipokuwa akimkimbia Sauli, hakumdhuru hata alipopata nafasi ya kumuua. Sio kwasababu sauli hakuwa mwovu machoni pa Daudi bali daudi alisema, 1Samweli 24:6 "Hasha! Nisimtendee bwana wangu, masihi wa BWANA, neno hili,kuunyosha mkono wangu juu yake,kwa maana yeye ni masihi wa BWANA" Daudi hakumdhuru Sauli kwasababu moja kubwa ni mpakwa mafuta.

Hakuna sheria hatari kama ya kupanda na kuvuna, unapomsema mtu vibaya kwa siri leo, siku moja utavuna tu hata kama sio leo. Kuwa makini kuwaongea watumishi wa Mungu vibaya. Ukimsikia mtu anaongea mwache ila wewe songa mbele kuihubiri injili, kuna watu wapo msukuleni, kuna watu wanateswa na shetani, kuna watu hawaijui kweli ya Kristo wewe songa mbele na siku ya mwisho ya hukumu, utang'aa sana.
Mchungaji Josephat Gwajima,

Share this article

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Copyright © 2015 HEZRON MWANAFUNZI WA YESU • All Rights Reserved.
Blogger Templates Design by BTDesigner • Powered by Blogger