MZIKI WA INJILI WAPATA KAMPUNI MPYA YA VIDEO.TAZAMA BEHIND THE SCENE YA UTENGENZEZAJI WA VIDEO YA LEVI NGOY.
Kijana wa nguvu katika mziki wa Gospel Levi Ngoy akiwa kwenye pozi la shooting.
Katika kuleta mabadiliko kwenye muziki wa injili hasa katika utengenezaji wa video za Gospel EAGLE VIEW PRO
imedhamiria kuleta mapinduzi mapya katika muonekano wa video za muziki
wa injili Tanzania.Ni kilio changu kila siku kupata kampuni mpya
zitakazoleta ubunifu na utofauti na video tulizo zizoea kuziona.Yapo
makampuni mengi ya video za Gospel yaliyo jitaidi kututoa tulikotoka
hadi sasa,lakini mpaka muda huu hakuna tofauti kubwa ya kusababisha
muziki wetu kupenya Kenya,Uganda,Rwanda na hata ulaya.
Habari Maalum,Mbc hot media,Ajm Production,Brayance media na Ltv ni
makampuni makubwa yenye majina hapa Tanzania yaliyosaidia kwa kiasi
kikubwa kuufikisha mziki wa Gospel hapa ulipo,lakini katika hilo zimekua
zikifanya kazi kama mazoea na kuto jali umuhimu wa kazi ya msani hasa
katika kuandaa Script,location,pamoja na kutafuta directors wazuri
watakao weza kusaidia kuongoza video katika utengenezaji ili mziki wetu
uweze kupenya katika nchi za nje na kusaidia waimbaji wa Gospel kuweza
kupata mialiko na hata kuingia kwenye tuzo za wenzetu.
Debro Gabriel ni
director mpya katika tasinia ya muziki wa injili aliye dhamiria kuleta
mapinduzi ya video za Gospel katika kizazi hiki kipya.Nimepata bahati ya
kutizama kazi zake naona tofautu kubwa ya video zake ambazo soon
kupitia Chomoza ya Clouds tv utakwenda kuziona mdau wangu.
Hii ni behind the scene ya utengenezaji wa video ya muimbaji wa mziki wa injili Levi Ngoy anaye kuja na album yenye jina 24-7 God Lives.
Director Debro Gabriel akiwa kikazi zaidi
Kazi ya shooting ikiendelea
Mdogo mdogo wataelewa...
On set Coco beach
Twende kaziii.
Warembo wa nguvu mdau wangu.Hapana chezea.











0 maoni:
Chapisha Maoni