UKOMBOZI KILIMANJARO HAUKWEPEKI
Ni kama vile dozi ya injili imeshauriwa na Daktari Bingwa, maana baada
ya uwanja wa mashujaa jijini Moshi mkoa wa Kilimanjaro kuhitimika kwa
mkutano mkubwa wa kanisa la Utukufu wa Yesu, sasa viwanja hivyo
vinapumua kwa siku chache tu kabla ya watumishi wengine kuendelea na
ratiba ua injili.
Zamu hii wakati Ufufuo na Uzima wakiwa kwenye jengo ambalo watakuwa
wakilitumia kama kanisa la mkoani humo, mtumishi wa Mungu kutoka Sweden,
Mwinjilisti Johannes Amritzer atapiga kambi kwa takriban siku tano,
kutakuwa na sherehe ya miujiza.
Pamoja na kuhubiri matendo makuu ya Mungu, waimbaji kadha wa kadha
watakuwepo wakiwemo Anne Annie, Kilimanjaro Gospel Choir, na wengineo
wengi. Kupanga kukosa ni sawa na kutoroka usipate uponyaji wako.

0 maoni:
Chapisha Maoni