“si juu ya damu na nyama bali ni juu ya falme na mamlaka juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho “{Wafeso 6:12}.Vita kali
Kuna watu
wengi wanaokata shauri
kumpokea YESU(wanaokoka).Kweli
wanakuwa wamepanga hasa
kwenda mbinguni.Wanaimba
nyimbo za sifa zionyeshazo hamu ya
kuwa YESU arudi upesi.Huaanza kushuhudia
kwa nguvu zote,hata kwa kufunga
na kuomba na machozi.Wanakuwa wameanza Vita
wanakutana na vikwazo na
shida njiani wanapigana sana.Wengi wanashinda lakini wengine wengi wanachoka polepole
na wanaachwa na
wenzao wanapobaki nyuma peke,
yao adui anakuja na kuwazunguka
na kuwateka mateka
Pengine
umekwisha waona hawa waliorudi nyuma wakaanguka.Usidhani kuwa mtu anayekata shaurikumwacha YESU huwa
wanajishtukia wameanguka kushindwa huku ni
sawa na usingizi.ukilala
kitandani unakuwa ukiwaza mambo
mengi au unazungumza na mwenzako.
La ajabu ni kwamba hujui unasinzia saa ngapi na dakika ngapi na ukaacha kusikia hata kama utalala ukiangalia saa unayezungumza naye anakuja kugundua kuwa anazungumza peke yake tu wewe unatambua kuwa ulikuwaumesinzia wakati unapoamka,
La ajabu ni kwamba hujui unasinzia saa ngapi na dakika ngapi na ukaacha kusikia hata kama utalala ukiangalia saa unayezungumza naye anakuja kugundua kuwa anazungumza peke yake tu wewe unatambua kuwa ulikuwaumesinzia wakati unapoamka,
ndivyo
ilivyo kwa maisha ya kiroho. Mtu
hawezi kujua lini hasa alipoanguka
Anakwenda taratibu hatua kwa
hatua akisogea nyuma na baadaye
anajikuta ameanguka amekwishatekwa na maadui
Maadui wetu
wana nguvu sana .Maadui hasa ni watatu
1. Adui wa kwanza ni shetani:
ni kawaida watu wa MUNGU kusema shetani ameshindwa Haleluya’’.Ni kweli Lakini hakufa ili kwa vile ameshindwa na YESU amri jeshi mkuu amekimbia na kuzungukazunguka akikuta mtu amebaki nyuma na amechoka basi anamteka tu Yeye shetani kama simba angurumaye huzungukazunguka akitafuta mtu ammeze -1 petro 5:8
Shetani siyo
mvivu anashughulika usiku na mchana akiwatafuta watu wa MUNGU ili aende
nao jehanamu Tusije tukasahau hili,
Biblia anasema kwamba tukeshe {tukae macho }
ili tumpinge atakapokuja kutushambulia.
Tuwe tumevaa silaha zote za MUNGU ili tupate kujikinga na kuzipinga hila zake {Wafeso 6:11}
2. Adui wa pili ni mwili:
Biblia inasema “mwili”, ina maana ya ule utu wa kale, ile hali ya dhambi tuliyonayo kwa asili.mwili hupambana na roho zetu Tena mwili huu {flesh} ni wa mauti.Paulo anaeleza vizuri jambo hili katika -Warumi 7:15-24
Upo
uwezekano wa kuishi kufuatana na mapenzi ya mwili k.m kutamani kuona wivu
kudanganya ili kukwepa hatari kutotii,n.k mwili upo karibu sana nasi tena ni
sehemu yetu.Ni adui wa hatari sana tumchunge
3. Adui wa tatu ni ulimwengu
Ulimwengu ni mambo yote yaliyo kinyume na MUNGU mambo
ya dunia k.m miundo ya jamii,siasa,mazingira,watu n.k
Ulimwengu una
dhiki BWANA hakutoa ahadi kwamba hatutapata dhiki -1thes.3:3,4
Dhiki ni sehemu ya ukristo wetu Lakini ni vigumu kuvumilia dhiki kama njaa,uchi,ugongwa na uchungu wa kifo.Hata hivyo ugumu huu siyo kisingizio cha kushindwa kwetu.
Dhiki ni sehemu ya ukristo wetu Lakini ni vigumu kuvumilia dhiki kama njaa,uchi,ugongwa na uchungu wa kifo.Hata hivyo ugumu huu siyo kisingizio cha kushindwa kwetu.
Ulimwengu
hauna dhiki tu.Una raha pia.Raha nayo inaweza kabisa kutufanya tumwache BWANA
kwa mfano Dema, ambaye Paulo alimwita mtendakazi pamoja nami alikaa na
Paulo muda mrefu akihubiri .Lakini Paulo alipo fungwa gerezani
tunashangaa tukiona anamwandikia mpendwa wake timotheo kwa masikitiko akisema
“DEMA aliniacha ,akiupenda ulimwengu huu wa sasa -2timotheo 4:10
Alikwepa
dhiki akakimbia raha wenzetu wengi wameangushwa na raha hizi kama mali,wapenzi,
vyeo n.k wanasahau kabisa wito waliloitwa na BWANA
Hata hivyo
maadui hawa wasitutishe.tunaye YESU,BWANA wa MAJESHI yule mwanamke aliyeitwa Hana,
alishuhudia akisema
Tunaweza kujiunga naye tukiimba
“Wala hakuna mwamba kama MUNGU wetu “ {1samweli 2:22}
Tunaweza kujiunga naye tukiimba
Moyo wangu
wamshangilia BWANA
Pembe yangu imetukuka katika BWANA
Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu
Kwa kuwa
naufurahia wokovo wako {1samweli 2:1}
Tujue tuko.
vitani vita vya kiroho, vya imani. tusiwe kama wajinga tukajisahau
Ndiyo maana
Paulo ,akijaa ROHO MTAKATIFU anatwambia ,
"Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za MUNGU mpate kuweza kushindana siku ya uovu ,mkiisha kuyatimiza yote ,kusimama “{efeso 6:13}
Katika
sehemu inayifuata, tujaribu kuona silaha hizi za MUNGU zitakazotuwezesha
kumshinda shetani, mwili na ulimwengu,
na kukua kiroho.
MUNGU awabariki sana ndugu wote.
Ni mimi ndugu yako Hezzo Daking
MUNGU awabariki sana ndugu wote.
Ni mimi ndugu yako Hezzo Daking

0 maoni:
Chapisha Maoni