Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe (wa
kwanza kushoto) akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya serikali.
Kajala Masanja (aliyeshika kijiko) akipakua chakula kwenye msiba wa rafiki yake kipenzi Wema Sepetu.
(PICHA: JELARD LUCAS, MAYASA MARIWATA NA BRIGHTON MASALU / GPL)
BABA mzazi wa staa wa sinema za Kibongo
ambaye pia ni Miss Tanzania 2006/2007 Wema Sepetu, Balozi Abraham Isaac
Sepetu ameagwa jioni ya leo nyumbani kwake Sinza - Mori jijini Dar es
Salaam.
Tukio hilo limehudhuria na viongozi
mbalimbali wa kiserikali akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph
Warioba, Getrude Mongela pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa Benard Membe na wengine wengi walifika kutoa heshima za
mwisho kwa mwili wa marehemu aliyefariki dunia Jumapili ya wiki
iliyopita.
Waziri Membe kwa niaba ya serikali ametoa
salamu za rambirambi na kuchangia kiasi cha shilingi milioni 1, “Kwa
niaba ya serikali tumechangia kiasi cha shilingi milioni 1. Hata mimi
pia nilimfahamu marehemu kwa muda mrefu na alikuwa kiongozi makini,
Mungu alilaze roho ya marehemu mahali pema peponi amen,” alisema Waziri
Membe.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kesho asubuhi kuelekea Zanzibar tayari kwa mazishi.
Uongozi wa Global Publishers LTD unatoa pole kwa wafamilia wote katika kipindi hiki kigumu. Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe!
Uongozi wa Global Publishers LTD unatoa pole kwa wafamilia wote katika kipindi hiki kigumu. Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe!












0 maoni:
Chapisha Maoni