Jumamosi, 26 Oktoba 2013

Unknown | 08:01 |
MIUJIZA NA MAAJABU INAENDELEA KUTOKEA KILA ITWAPO LEO.MAMA MMOJA APONA UKIMWI NA SASA AMUA KUMWIMBIA MUNGU SIFA
Mama huyu ndiye aliyepona virus na ukimwi
Tumbo hili lilikuwa limevimba lakini sasa tumbo liko safi na amepona
Mama akiendelea sana kutoa stori jinsi alivyotendewa miujiza na Mungu.
Tazama kiganja chake ambavyo kimepona na hakina magamba pia hakuna madonda

Ndugu yangu haijalishi unapitia katika hali gani au tatizo gani kubwa la kimaisha au uchumi,bado kwa Mungu inawezekana,kupona kutajirika au kuvuka hali hiyo,hivyo nakutia moyo mtafute Mungu maadam anapatikana pia jifunze kuomba sana hasa unaposikia mikesha na mifungo itakusaidia kwa maana wote waliofanikiwa waliamua kumlilia Mungu kwa kufunga na kuomba.Jaribu leo utashinda.YEREMIA 32:27 BAADA YA KUOKOKA AMEACHA USAGAJI

Kumekuwa na shuhuda nyingi kuvutia na kusababisha wengine kuinuliwa imani yao na wengine kuwa na wasiwasi na washuhudiaji kama kweli wameacha yale mambo waliyoyafanya kabla hawajampokea Bwana Yesu.

Leo kuna ushuhuda wa dada Janeth Boynes aliyekuwa msagaji na kufikia hatua ya kuoa mwanamke mwenzake kabla Bwana Yesu hajamuita na kuacha usagaji ili amtumikie, Janeth tangu akiwa na miaka 12 mpaka alipoenda chuoni, alikuwa akiendelea kutumia madawa ya kulevya na kubeba uchungu alioumizwa na wavulana na kujikuta akivutia wanawake.

Siku moja alipoenda dukani alikutana na mwanamke akaanza kumwambia habari za Bwana Yesu na kumwalika kanisani na kukutana na akina dada wengine na Janeth akawaambia tatizo lake hivyo anahitaji kuacha usagaji aishi kwa ajili ya Bwana Yesu.

Waliweza kumsaidia na kumuombea Mungu ambadilishe baada ya muda, Mungu aliuponya moyo wake na kubadilisha aina ya maisha aliyokuwa akiishi.

Hivi sasa Janeth amekuwa msaada kwa wadada wote waliopitia hali kama yake na kuwashuhudia upendo wa Kristo kwamba unaweza kuondoa madhaifu yote na kukombolewa kabisa. “Haikuwa kazi rahisi lakini kwa uwezo wa Roho Mtakatifu niliweza kuachana na tabia nilikuwa nazo na kuwa msaada kwa wengine”

Je mtu kushuhudia mbele za watu kwamba alikuwa msagaji, shoga, jambazi, mzinzi aliye kubuhu, mchawi nakadhalika. Ni Muhimu kushuhudia kila jambo? au unaweza kufunguliwa katika hayo na ukawa ukimshukuru Mungu kisiri siri.

-----------------------------------------------------------------------------
ANUSURIKA KIFO CHA CHATU.
 Unaweza usiamini haraka unapokutana na ushuhuda wa mtu aliyenusurika kifo cha kumezwa na chatu na baadaye tena kutafunwa na mamba, lakini hivi sasa ni mmoja wa watumishi wa Mungu anayehubiri Injili na kuvuta watu wengi kwa Yesu.

Mikasa hiyo ilimkumba Mwinjilisti Goodluck Kessy wa huduma ya Maombezi ya ELOHIM iliyoko Jijini Arusha, ambaye alilazimika kufanya hafla maalum ya kumshukuru Mungu kwa kumnusuru na kifo, Gazeti hili likiwa moja ya walioalikwa katika hafla hiyo.

Mwinjilisti Kessy alitoa ushuhuda huo ofisini kwake eneo la Kijenge Mwanama Jijini Arusha wakati wa halfa hiyo ambayo ilikwenda sambamba na kutimiza miaka 24 ya huduma yake ya ELOHIM.
Alisema kutokana na jinsi Mungu alivyomlinda na kufanikisha huduma yake kwa kipindi chote hicho, ameamua kwa dhati kumpa maisha yake na kumtumikia kwa bidii.

Akizungumzia jinsi alivyonusurika kifo cha kutafunwa na mamba, alisema anakumbuka siku moja akiwa mtoni Mkoani Morogoro alikamatwa na mamba lakini akafanikiwa kujikwamua kutoka kinywani kwa mnyama huyo.
“Nakumbuka tena siku nyingine nikiwa porini Mkoani Mbeya nilikutana na chatu aliyenivamia na kuanza kujivingirisha mwilini mwangu lakini katika hali ya ajabu nilipambana naye hadi akaniachia na kutokomea porini humo”, alisema Mwinjilisti Kessy.

Alisema kuwa anaamini Mungu alikuwa na makusudi maalum ya kumuokoa na kifo ambayo ni kumuingiza katika utumishi anaoufanya hivi sasa wa kuhubiri Injili na kuujenga ufalme wa Mungu.
Mwinjilisti Kessy alisema huduma ya ELOHIM anayoiongoza imekuwa msaada kwa watu wengi wenye matatizo mbalimbali ya vifungo vya giza, ambapo Mungu huwafungua na kuwaweka huru
Naye Mwana Maombi aliyefahamika kwa jina la Bi. Onesmo Olotu alimshukuru Mungu kwa kumponya vidonda vya tumbo vilivyomsumbua kwa muda mrefu kupitia huduma ya maombi inayofanywa na Mwinjilisti Kessy

Bi. Onesmo alisema kuwa vidonda vya tumbo vilimsumbua kwa muda mrefu lakini baada ya maombi amepona na anaendelea kumsifu, kumuabudu na kumtumikia Mungu.
source-Msemakweli.

 ---------------------------------------------------------------------------------

Hizi ni Siku Za Mwisho, Kijana Amuoa Mama Yake Mzazi.




Biblia inaposema siku za mwisho kutakuwa na mengi basi hili nalo pole pole utaliona Tanzania. Ukistaajabu ya Mussa Kugeuza fimbo kuwa nyoka basi utashangaa ya Filauni a.k.a Farao nae kugeuza fimbo kuwa nyoka. Maajabu huwa hayaishi dunia Katika kijiji kiitwacho Sleepy a.k.a usingizi kilicho katika wilaya ya Slovo Park karibu Siyabuswa Kusini mwa Afrika, yametokea ya kutokea watu wameshuhudia mtu akila kiapo na mama yake mzazi kuwa watapendana katika hali njema ama mbaya katika umasikini ama utajiri. Kwa maneno mepesi wamefanya nadhiri ya ndoa


Kijana huyo ambaye ni "Karumanjila" ama  mganga wa jadi kutoka Siyabuswa katika eneo maarufu la Mpumalanga, alisema  katika sherehe ya harusi hiyo kuwa ndoa ya yeye na mama yake ni kutuliza hasira za mababu zake ambao bado wamemkasirikia baba yake kwa kumuacha mama huyo. Na anajivunia kumuita mama yake "Mke"


Siku hiyo ya  Jumapili zaidi ya watu 2000  walifika kushuhudia harusi ya Buti Mphethi, 28,kwa mama yake Francinah Makunyane, 62. Kweli duniani hamnazo.


Mphethi alisema kuwa "Waungwana" walikuwa wamemuagiza kulipa lobola yaani mahali kwenye familiaya mama yake yaani kwa babu zake na wajomba zake ili aweze kumuoa mke wake yaani mama yake ambaye kwa sasa ameachana na baba yake (Buti).


Mphethi  ambaye amepaswa kulipwa lobola wa ng'ombe wawili kwa ajili ya kumuoa mama yake  pamoja na kulipa mijihela  R14 000 sawa na shilingi kama 280,000 kwa hela za kibongo.


Harusi hiyo ambayo kwa mila za jamii hiyo ilianza siku ya jumamosi nyumbani kwa mama yake na buti ili kumfanyia Send Off na kisha Sherehe kufanyika Jumapili nyumbani kwa Buti mwenyewe.


Mphethi ambaye ameacha masomo yake ya mwaka wa pili alipokuwa akisoma "Sound Engineeering"  katika Chuo Kikuu Tshwane Technology  mwaka 2003 na kuitikia wito wa kuwa Kalumanzira a.k.a Sangoma. Buti Yeye anahesabu ni kama wito kutoka kwa mababu zake.




Mphethi alisema kuwa baba yake William Mphethi alikuwa bado hai, na alikuwa na wake wanne. Baba yake huyo anakaa na mke wa Mzee katika kijiji cha Burgersfort huko Limpopo.

------------------------------------------------------------------
 BAADA YA MIAKA 21 YA NDOA MCH BRUNO MWAKIBOLWA APATA MTOTO
Mch Bruno Mwakibolwa Kushoto akiwa mtaani na Mmoja wa washirika wake Bw Masanja Mkandamizaji wakihubiri Injili, Mchungaji Mwakibolwa hutimia gari lake binafsi pichani aina ya Fuso kuzunguka mitaani na kuhubiri

Askofu Bruno Mwakiborwa wa kanisa la Evangelical Assemblies Of  God Tanzania(EAGT), ambaye pia ni Mchungaji kiongozi wa kanisa la Mito ya Baraka lililoko maeneo ya Jangwani jijini Dar es Salaam, amefanikiwa kupata Zawadi ya mtoto wa kike toka kwa Mungu waliyempa jina  la “Gwandumi” yaani Malaika.

Akitoa shukrani hizo mbele ya kanisa akiwa pamoja na mkewe, Mchungaji Mwakiborwa  mwenye umri wa miaka 59 alisema mnamo tarehe 26-12-1990 miezi miwili mara baada ya kuokoka Mungu alimwambia kuwa atampa mtoto wa kike , na jina lake atamwita Gwandumi kwa kiswahili Malaika ahadi ambayo haikuwa rahisi kuiamini kwa kuwa alikuwa mchanga kiroho lakini aliamini hivyo kwa kuwa Bwana ndio alisema.


Baada ya miaka mingi kupita, mwaka jana 2010 akiwa nchini Israel Katika jiji la Jerusalemu wakati wa kutoa sadaka, aliamua kumtolea Mungu SADAKA ya Dola za Kimarekani Mia Moja (100). Baada ya  sadaka hiyo kwa kuwa alikuwa na maombi ya uchungu juu ya hilo ndipo Bwana Yesu akamwambia “Nimesikia Maombi yako”.


Tarehe 31/05/2011 ikiwa ni miezi tisa toka atoe sadaka kwa Bwana ndipo mtoto akazaliwa katika Hospitali ya Regent iliyoko Upanga jijini Dar es salaam. Akasema kwa mtu aliyeokoa ni vizuri unapofanya maombi, hakikisha unapeleka na sadaka kwa Mungu.
-----------------------------------------------------------------
 Testimony: Albert G Sengo amshukuru Mungu Kwa Kumponya Mwanae aliyemeza COIN ya shilingi Hamsini


Albert G Sengo
Albert G Sengo ni mtangazaji wa Kituo cha Clouds Fm jijini Mwanza na mdau, hivi karibuni amemshukuru Mungu kwa kumuokoa mwanaye aliyemeza coin ya shilingi Hamsini. Sengo alisema  

Ilikuwa ni asubuhi ya Jumatatu ya tarehe 27juni2011 nikiwa na plani za kuamka saa 3 mara baada ya uchovu wa pilika pilika za siku iliyopita yaani Fiesta Mwanza stimu za usingizi zilikatika ghafla mara baada ya mke wangu kunipa taarifa kuwa my second kid Cuthbert aka Obama(3) kameza sarafu ya shilingi 50.

Huduma ya kwanza ilikuwa nikumuuliza yu hali gani na anajisikiaje:

Jibu: "nimemeza hela kama wali"
Swali: iko wapi?
Jibu: "nimetupa humu.." akielekeza kidole mdomoni
Swali: sasaaa.. huumiii?
Jibu: "mmh-mmh" akimaanisha kukataa

Ndipo pilika zikaanza kutafuta daktari ambaye alishauri kumpeleka hospitali kufanyiwa uchunguzi. Tulipita hospitali kadhaa bila mafanikio nyingi zikiwa hazitoi huduma ya X-ray kutokana na tatizo la mgao wa umeme linaloendelea nchini.

Huku na huko hatimaye tuakapata huduma ya X-ray katika hospitali binafsi inayoitwa 'Mwananchi' iliyoko wilaya ya Nyamagana mitaa ya Makoroboi nayo ikaonyesha sehemu sarafu hiyo ilipofika, madaktari wakasema kuwa ipo katika eneo lisilo la mashaka sana (kwenye utumbo kifuani) hivyo tumrudishe siku ya pili kama hatakuwa ameitoa kwa njia ya haja kubwa.

Siku ya pili X-ray ikafanyika na kuonyesha kama inavyoonekana pichani juu. Nao madaktari wakasema kuwa ipo kwenye utumbo imeshuka kidogo chini ya mbavu hivyo akatupa siku mbili kurejea kama haitakuwa imetoka. Kweli baada ya siku mbili .... Ikatoka.

Ashukuriwe MUNGU muumba wa mbingu na nchi.
  

X-Ray ikionyesha shilingi Hamsini ndani ya Tumbo


 ---------------------------------------------------------------------------------
 PRECIOUS GROUP WATEMBELEA MUHIMBILI.
 Mtoto ambaye ameathirika vibaya sana,Mama wa mtoto huyu alikuwa na upungufu wa madini ya Folic Acid na ndiyo ikapelekea kujifungua mtoto huyu.Madini hayo yanapatikana kwenye vyakula fresha kama bamia,matembele na matunda yote
 Unaweza kuanza kutumia vidonge vya Folic Acid miezi mitatu kabla ya kubeba ujauzito au hata mtoto mwenye umri kuanzia miaka 10,na wakato wowote kwa mama ambaye hatumii njia za uzazi wa mpango ama mara baada ya kuachana na njia hizo..na zinapatika maduka yote ya dawa na kwa bei nafuu zaidi ya Panadol
 Mmoja wa watoto walioathirika na tatizo
Moja wapo ya tatizo linalochangia matatizo haya ni mimba za utotoni kama mama wa mtoto huyu na pia kuficha mimba hivyo kutokwenda hospital mapema ili kuweza kugundua tatizo..,hivyo tunashauriwa kuepukamimba hizo na kuzidi kutoa Elimu mashuleni na kwa familia zetu ili wajue tatizo hili na jinsi yakujifunza .


Kijana Raphael Steven (18) mkazi wa Mwangata katika Manispaa ya Iringa akiwa amejinyonga kwa kutumia kanga ndani ya chumba cha mama yake mzazi usiku huu

                                Naomba Radhi Kwa Picha hizi
Umati wa wananchi wa Mwangata wakitazama mwili wa kijana huyo
Ujumbe mzito alioacha kijana huyo kabla ya kujiua wakutwa ndani ya chumba chake
Dawa ya kuua wadudu ambayo alikuwa amedai kuwa amekwenda kuipulizia ndani ya chumba cha mama yake
 
Kijana Raphael Steven (kushoto) enzi za uhai wake akiwa na rafiki yake
  
Vilio na simanzi zimetanda katika eneo la Mwangata katika Manispaa ya Iringa kufuatia kifo cha kijana Raphael Steven (18) ambaye alikuwa akijishughulisha na kazi ya kusajili laini za kampuni ya Tigo mjini Iringa ,kufuatia uamuzi wake wa kukatisha maisha yake kwa kujinyonga kwa kutumia kipande cha kanga ya mama yake mzazi ndani ya chumba cha mama yake huyo.

Tukio hilo ambalo limeacha maswali kwa wananchi wa Mwangata huku baadhi yao wakishindwa kujizuia kumwaga machozi limetokea usiku huu majira ya saa 9 hivi baada ya mama mzazi wa kijana huyo kubaini kijana wake huyo akining'inia katika chumbani kwake baada ya kujinyonga .


Ndugu wa karibu na kijana huyo walidai kuwa majira ya saa 2 usiku alimuaga bibi yake kuwa anaingia chumbani kwa mama yake mzazi kwa ajili ya kumsaidia kupulizia dawa ya kuua mbu na kuwa  mbali ya kukatazwa kuingia chumbani kwa mama yake bado alilazimisha kuingia kuifanya kazi hiyo.

Inadaiwa kuwa baada ya kuingia katika chumba hicho aliufunga mlango kwa ndani ya kuigiza kupuuliza dawa ila kutokana na masaa kuzidi kuyoyoma bila kutoka ndipo walipoamua kusukuma mlango na kumwona kijana huyo akiwa amekufa kwa kujinyonga kwa kamba hiyo ya upande wa kanga ya mamake mzazi.

Kijana huyo mbali ya kuufunga mlango pia aliiharibu taa ya ndani ya chumba hicho na kupelekea chumba chote kuwa giza na kuchukua dumu tupu na kusimamia katika paa ya nyumba hiyo na kuifunga kamba hiyo na baada ya kuingiza shingo yake katika kitanzi hicho alilisukuma dumu hilo na kuanguka chini na yeye kubaki akining'inia juu na kufa.

Mashuhuda walioteta na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com walidai kuwa kijana huyo mchana wa leo alionekana mtaani akiwa na mawazo tele na hakuna na muda wa kuzungumza na mtu kama siku za mwanzo .

Hata hivyo mashuhuda hao walisema kuwa kwa siku ya jana kijana huyo alionekana katika ukumbi mmoja wa starehe na kuzuiwa kuingia katika ukumbi huo baada ya kukosa kadi ya mwaliko .

Habari zinadai kuwa kijana huyo alikuwa hana makuu na mtu na kuwa siku zote alikuwa ni kijana mwenye kuheshimu wakubwa na wadogo na kuwa hata kifo chake bado kinaacha maswali kwa wananchi wa eneo hilo.

Zipo habari zinazodai kuwa kijana huyo amekufa kifo kama kile cha baba yake mzazi aliyekufa kwa kujinyonga mwaka 2002 kwa wakati huo walikuwa wakiishi eneo la Isoka mjini Iringa.

Mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com umebaini kukuta ujumbe wa maandishi ambao marehemu huyo alipata kuuacha kabla ya kifo chake katika meza ya chumba chake na katika ujumbe huo amepata kuacha maneno mazito yakiwemo ya kutaka asisumbuliwe mtu yeyote kwa kifo chake na kuwa kuwaaga baadhi ya marafiki na mpenzi wake mmoja pamoja na mama yake mzazi na kudai kuwa maisha ya Dunia Jembe lenu natangulia nilikotokea.

"Asisumbuliwe mtu kwa kifo changu na na kutaja majina ya rafiki zake na mpenzi wake (ambayo yamehifadhiwa huku akimalizika na neno .Respect..Don't Cry Momy and Rukia!!...Pole mama nimeamua kumfuata baba angu!!" ulisomeka ujumbe huo ambao ameacha marehemu
Nina swali langu.Je nini kitafata huko mbinguni??
---------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Unaweza kupagundua mahali hapa? hivi watu wa mipango miji wanajua madhara ya kuruhusu ujenzi wa namna hii?ebu wadau wasilisheni hoja maana kila nikikumbuka kile kilichotokea katika soko la mwanjerwa moyo wangu huruka kichurachura
BEATRICE DAVID MWENDAPOLE
Ni Dada ambae ukikutana nae uwezi amini kuna changamoto/Majaribu,Shida na taabu alipita.Beatrice ni Mama mwenye watoto wawili wakubwa alio zaa akiwa na umri wamiaka 18.Mwaka 1993 Mama yake mzazi alifariki Dunia na Baadae mwaka 1999 Baba yake mzazi alifariki.
Beatrice 
Baada ya wazazi kufariki alipitia shida yakuto kuelewana na Kaka yake Mkubwa ambae mpaka sasa awaongei pamoja.Wazazi wao waliwaacha wakiwa watatu,Mvulana mmoja na mabinti wa wili.Kuto kuelewana uko kulitokana na Kaka yake kutaka kuuza nyumba bila kuwashirikisha.

Ugomvi huu ulidumu kwa takribani kwa miaka 7.Lakini kupitia maombi ya Dada huyu alie amini mtetezi wa Maisha yake ni Mungu alipigana nakuakikisha nyumba haiuzwi.Ukiachilia mbali ugomvi wa Kaka yake,Maisha yalibadilika nakuwa magumu sana kwani kuna wakati alishindwa kuwalea watoto wake kutokana nakuto kuwa na kazi.
Lakini katika haliyote hiyo akuacha kumlilia Mungu awe mtetezi wa Maisha yake hasa watoto wake.Kuna wakati alilala njaa na watoto wake bila kupata msaada kwa ndugu yeyote.
Beatrice akifanya maojiano na Blogger Uncle Jimmy.
Anaendelea kueleza hali ya Maisha ilikuwa ngumu nakufikia sehemu yakutaka kukata tamaa yakuishi.Marafiki,Majirani,Ndugu walimtenga kisa wokovu.Mwaka 2010 akiwa katika hali hiyo alifanyikiwa kupata pesa kidogo aliokuwa akiipata katika kodi ya wapangaji walio wapangisha katika nyumba walio waachia Marehemu wazazi wake.
Ndipo Beatrice akapata wazo lakusomea uwandishi wa habari nakufanyikiwa kumaliza kozi iyo na sasa ni mwandishi katika Magazeti ya jamii.

Anakutia moyo ndugu msomaji akuna jambo gumu lakumshinda Mungu.Unapo pitia majaribu yoyote mwamini mungu ndie mtetezi wa Maisha yako


Share this article

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Copyright © 2015 HEZRON MWANAFUNZI WA YESU • All Rights Reserved.
Blogger Templates Design by BTDesigner • Powered by Blogger