Alhamisi, 24 Oktoba 2013

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI HEZZO DAKING ANAJIANDAA KUJA NA ALBUM MPYA INAYOSEMA" YESU NI MSHINDI".

Unknown | 05:01 |

CHIDUMULE COSMAS
Sauti ilinisimbua sana hata baada ya kufika Dodoma. Tulipofika ukumbini sikuwa na hamu ya kuimba, Remmy akaona nimenyong'onyea akanipa glasi ya konyagi ili itoe nishai, ikanidondoka na kuvunjika. Nikakimbia stejini maana toka kwenye glasi ile kulitoka upanga au mkuki. Nikarudi Dar es Salaam asubuhi iliyofuata, nikatangaza radioni, BASATA, na kwa bendi yangu kwamba mimi nimeamua kumfuata Mungu, nimeokoka."

"Ibada ni mawasiliano yako na Mungu, si kwenda kanisani wala msikitini. Mawasiliano kati ya nafsi ya ndani na Mungu, tofauti na leo mwili ndio umekuwa muhimu kuliko nafsi. Ninao marafiki ambao hawajaokoka lakini wote nawapa heshima ile waliyopewa na Mungu."

"Muziki wangu umenipa umaarufu lakini bado sijafaidika kama muuzaji wa muziki wangu anavyofaidika. Kwa mfano ukiniproduce kwa milioni 3 ukisharudisha fedha hiyo tuingie mkataba mwingine mpya wa namna ya kugawana mapato hayo lakini hiyo ni tofauti. Utakuta mtu anauza kazi yako hata baada ya miaka mitano na bado hupati chochote, wakati yeye ananunua magari na kujenga nyumba.

"Ujumbe wangu kwa wanamuziki wenzangu ni kuishi maisha halisi ili kila mtu avunwe na Mungu akiwa ameshakomaa, hakuna sababu ya kufa na kijana mdogo bila sababu za msingi."


Share this article

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Copyright © 2015 HEZRON MWANAFUNZI WA YESU • All Rights Reserved.
Blogger Templates Design by BTDesigner • Powered by Blogger